Tuesday, 19 September 2017

HIZI NDIZO BASI MPYA ZA DAR LUX.

Kampuni ya Dar lux imeweza kuwajali wasafiri wake kwa kuwaletea basi mpya 10 aina ya Higer kutoka nchini china.
Aidha katika basi hizo kuna
basi za luxury zaidi ambazo zimekuja na madaraja mawili ndani ya basi moja.


Mabasi hayo yana sehemu ya V.I.P ambayo inamfumo wa siti wa 2 kwa 1 na kila siti ikiwa na tv yake pamoja na sehemu ya kuchajia simu kwa njia ya USB. Aidha katika sehemu ya V.I.P kuna jumla ya siti tisa.
Katika sehemu ya pili ambayo ni sehemu ya kawaida kuna mfumo wa siti wa 2 kwa 2 kukiwa na tv 5 ambazo ziko juu huku kukiwa na USB kwa ajili ya kuchajia simu. Katika basi hizo pia kuna huduma ya choo ambayo itakufanya uweze kujisaidia haja ndogo uwapo safarini.

 
Muonekano wa sehemu ya kwanza V.I.P class

Siti ya abiria katika V.I.P section.



Sehemu ya pili ya basi "ECONOMY CLASS".

Choo cha basi ya Dar Lux.
Mabasi hayo yanatarajiwa kuanza safari hivi karibuni kuendelea na safari zake katika barabara za Dar es salaam Mbeya, Dar es salaam Kahama, Dar es salaam Mwanza na Dar es salaam Nairobi.


No comments:

Post a Comment

KILIMANJARO EXPRESS ANAFUNGA MWAKA KIANA YAKE.

Kampuni ya usafirishaji wa abiria iliyojikita katika ruti ya majiji mawili ya Dar es salaam Arusha imekuja kitofauti zaidi baada ya kununua ...