Abiria waliokuwa safarini na basi la kampuni ya Rungwe Express lenye namba za usajili T 992 DJW lililokuwa linatokea jijini Mbeya
kuelekea jijini Dar Es Salaam wamenusurika kifo baada ya basi hilo kupata ajali.
Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa lori ambalo lilikuwa mbele yao dereva wa basi alikuwa analipita ghafla akakutana na lori lililobeba kontena mbele ikabidi dereva aende pembeni ili kuepusha kugongana uso kwa uso.
Katika ajali hiyo hakuna vifo wala majeruhi zaidi ya basi kuharibika tu.



No comments:
Post a Comment